Saturday, April 7, 2012

Tagged Under:

Je...Lulu ahusika kifo cha Steve Kanumba

By: Chris Wasonga On: 6:57:00 AM
 • Share The Gag
 • Ndugu wa Kanumba akihojiwa


  TAARIFA kutoka kwa ndugu wa Marehemu Steven Kanumba ambaye alikuwa akiishi nae Sinza jijini Dar es Salaam na wakati mauti yanamkuta Kanumba alikuwapo nyumbani hapo zinasema chanzo cha kifo chake ni ugomvi baina ya kanumba na Msanii mwingine wa kike ambaye ni rafiki yake.

  Ndugu huyo amepasha kwa wanahabri kuwa Msanii huyo wa kike ambaye analikuwa na mahusinao na marehemu kuwa ni Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu.

  Akisimulia kwa ufupi chanzo cha kifo hicho cha Ghafla cha Nguli wa Filamu za Kibongo “ Bongo Movie” anasema wakiwa hapo nyumbani alifika Lulu majira ya usiku.

  Anasema aliwaacha wawili hao wakizungumza klakini baade alisikia kuwepo kwa malumbano na wakahamia chumbani ugomvi ukazidi kuendelea.   0 maoni:

  Post a Comment