Sunday, January 29, 2012
Saturday, January 28, 2012
Kadi za Harusi
For a card like this costing 2,500/= delivery after 3 days call us today Kariwe card design 022 2420042, 0753 447977/ 022 2420042 |
Kwa kadi kama hii pamoja na boxi yake tunauza kwa shillingi 3000/- Piga simu leo upate kadi baada ya siku tatu. Kiriwe Education Supplies, 0753 447 977, 0654413 694 emil: kiriweedu@yahoo.com |
By:
Unknown
On 2:32:00 AM
Friday, January 13, 2012
BIBI HARUSI NA SALOON
ILI kuziweka nywele zako katika muonekano wa kupendeza katika siku maalumu kama ya harusi, unapaswa kuzingatia mambo mbalimbali kama nitakavyoyaeleza katika safu hii leo.
Miongoni mwa mambo hayo, ni kufuata maelekezo ya wataalamu kuhusu suala zima la matunzo ya nywele zako.
Wapo ambao wamekuwa wakitunza au kutengeneza nywele zao kwa kuiga wenzi wao, jambo ambalo wakati mwingine husababisha madhara na kuhatarisha maisha ya nywele za mhusika.
Pia wapo ambao imekuwa ni mtihani kwao, kutofautisha namna ya utumiaji na uboreshaji wa mitindo wakati wa kawaida na wakati maalumu. Kwa kutambua hilo, tumeamua kukuletea baadhi ya dondoo zitakazokufanya kuwa na nywele zenye muonekano wa kuvutia katika siku maalumu kama ifuatavyo;
Elewa unachokitaka; Pamoja na kuwa mtaalamu wa mitindo ya nywele hutegemewa sana katika zoezi hili. Mchango wako ni muhimu sana katika kumuongoza na kufikia muonekano unaokusudia.Wakati mwingine ikiwa unashindwa kumwelekeza, ni bora kutumia picha kumuonyesha jinsi unavyopenda kuonekana, hii itampa nafasi ya kukushauri.
Kwa kuwa unatakiwa kutumia mtindo maalumu, ambao unaendana na mavazi yako. Si vibaya ukapita kwa mtaalamu wako wa siku za nyuma na kumpa wazo lako, ikiwezekana aanze kulifanyia kazi kwani mitindo kama hiyo hupendeza zaidi ikiwa mtaalamu atajiandaa mapema.
Usioshe nywele zako kwenye siku ya tukio: Ikiwa unatengeneza nywele maalumu kwa ajili ya siku maalumu , unashauriwa kuzisafisha siku moja kabla. Hii itasaidia kuonyesha uhalisia wake. Pia kuonyesha uchangamfu wake. Wakati mwingine uoshaji nywele huchangia kuzifanya zisinyae.
Hakikisha unavaa blauzi au fulana yenye shingo kubwa, wakati wa kwenda kutengeneza nywele zako. Hii ni muhimu hasa ikiwa utabadilisha nguo . Kwani kwa kufanya hivyo itakupa wepesi wakati wa kuvua nguo. Vinginevyo unaweza kuharibu mtindo wako.
Tumia mapambo kuboresha zaidi muonekano wa nywele zako: Unashauriwa kutumia mapambo yanayoendana na rangi ya mavazi yako.
Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya Email: maikube@yahoo.co.uk
By:
Unknown
On 4:47:00 AM
Thursday, January 12, 2012
Tuesday, January 10, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)