To place an advert or if you have any relevant article you would want us to publish kindly contact us on this no. +255768191019/ +255716583496 or drop us an email @ mail.harusinzuri@gmail.com. Thanks alot for visiting this blog.

Friday, January 13, 2012

BIBI HARUSI NA SALOON

4:47:00 AM



ILI kuziweka nywele zako katika muonekano  wa kupendeza katika siku maalumu  kama ya harusi, unapaswa kuzingatia mambo mbalimbali kama nitakavyoyaeleza katika safu hii leo.  

Miongoni mwa mambo hayo, ni kufuata maelekezo ya wataalamu kuhusu suala zima la matunzo ya nywele  zako.
Wapo ambao wamekuwa wakitunza au kutengeneza nywele zao kwa kuiga wenzi wao, jambo ambalo wakati mwingine husababisha madhara na kuhatarisha maisha ya nywele za mhusika.

Pia wapo ambao imekuwa ni mtihani kwao, kutofautisha namna ya utumiaji na uboreshaji wa mitindo wakati wa kawaida na wakati maalumu. Kwa kutambua hilo, tumeamua kukuletea baadhi ya dondoo zitakazokufanya  kuwa na nywele zenye muonekano wa kuvutia katika siku maalumu kama ifuatavyo;

  Elewa unachokitaka;  Pamoja na kuwa mtaalamu wa mitindo ya nywele hutegemewa sana katika zoezi hili. Mchango wako ni muhimu sana katika kumuongoza na kufikia muonekano unaokusudia.Wakati mwingine ikiwa unashindwa kumwelekeza, ni bora kutumia picha kumuonyesha jinsi unavyopenda kuonekana, hii itampa nafasi ya kukushauri.

Kwa kuwa unatakiwa kutumia mtindo maalumu, ambao unaendana na mavazi yako. Si vibaya ukapita kwa mtaalamu wako wa  siku  za nyuma na kumpa wazo lako, ikiwezekana aanze kulifanyia kazi kwani mitindo kama hiyo hupendeza zaidi ikiwa mtaalamu atajiandaa mapema.
Usioshe nywele zako kwenye siku ya tukio:  Ikiwa unatengeneza nywele maalumu  kwa ajili ya siku maalumu , unashauriwa kuzisafisha siku moja kabla. Hii itasaidia kuonyesha uhalisia wake. Pia kuonyesha uchangamfu wake.  Wakati mwingine uoshaji nywele huchangia kuzifanya zisinyae.  

Hakikisha unavaa blauzi au fulana yenye shingo kubwa, wakati wa kwenda kutengeneza nywele zako. Hii ni muhimu hasa ikiwa utabadilisha nguo .  Kwani kwa kufanya hivyo itakupa wepesi wakati wa kuvua nguo. Vinginevyo unaweza kuharibu mtindo wako.

Tumia  mapambo kuboresha zaidi muonekano wa nywele zako:  Unashauriwa kutumia mapambo yanayoendana na rangi ya mavazi yako.
Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya Email: maikube@yahoo.co.uk

Written by

We are Creative Blogger Theme Wavers which provides user friendly, effective and easy to use themes. Each support has free and providing HD support screen casting.

1 maoni:

  1. Keep up with the goog job that you are doing.

    ReplyDelete

 

© 2013 Harusinzuri. All rights resevered. Designed by Templateism

Back To Top